15 August 2013

WAFUASI WA SHEKHE PONDA WATAKA UHURU



 Na Rachel Balama
MA H A K A M A K u u Kanda ya Dar es Salaam imeombwa kutengua hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu dhidi ya wafuasi 52 wa Shekhe Ponda Issa Ponda, waliohukumiwa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela.

Kwa kuwa, hakuna ushahidi wa kuonesha kwamba washtakiwa hao waliandamana isipokuwa hakimu aliwatia hatiani kutokana na kujiridhisha kwamba washtakiwa walitenda kosa wakati anaandika hukumu.
Wafungwa hao, kupitia wakili wao, Mohamed Tibanyendela wanapinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu ambapo pamoja na mambo mengine, wanadai hakimu hakuzingatia matakwa ya msingi kisheria ili kuwatia washtakiwa hatiani.
Akiwasilisha rufaa hiyo jana mbele ya Jaji Salvatory Bongole, wakili Tibanyendela alidai, hakimu hakuwa na ushahidi wa kujiridhisha kwamba kulikuwa na njama za kukubaliana kutenda kosa miongoni mwa washtakiwa na badala yake alikuwa na dhamira ya kuwatia hatiani wakati akiandika hukumu hiyo.
Alidai, hukumu iliyotolewa na ushahidi uliorekodiwa una upungufu mkubwa kwenye ushahidi wa Serikali hivyo hakukuwa na msingi wowote wa kiushahidi kisheria wa kuweza kuwatia hatiani washtakiwa.
Alidai, katika hukumu hiyo mwongozo wa kuandika hukumu kisheria haukufuatwa na badala yake washtakiwa wote waliingizwa kwenye kundi moja na kutiwa hatiani kwa makosa yote bila kuchambua vifungu vya sheria kwa makosa waliyoshtakiwa nayo.
Wakili alidai hakimu alishindwa kuchambua ushahidi uliotolewa mbele yake, ni dhahiri kwamba hakimu alitoa hukumu bila kubainisha anawatia hatiani washtakiwa kwa sheria ipi.
Alidai, katika hukumu hiyo ushahidi haujajitosheleza isipokuwa hakimu alitengeneza ushahidi wake kwa kuwa alikuwa na dhamira yake ya kuwatia hatiani washtakiwa kabla ya hukumu.
Aliendelea kudai kuwa, vitu kama panga, visu, mabango na vinginevyo haviwezi kuthibitisha kosa lilifanyika ambapo kwa ushahidi uliotolewa na washtakiwa unaonesha kwamba baadhi ya washtakiwa walio waongoza polisi kwenda kuwakamata washtakiwa wengine na washtakiwa hao hawakukamatwa wakati mmoja.
Pia wanadai kuwa, katika hukumu hiyo, hakimu alijikanganya kwa kumwachia huru mmoja wa washtakiwa na kuwatia hatiani washtakiwa wengine.
Machi, mwaka huu, Hakimu Sundi Fimbo wa Mahakama ya Kisutu aliwahukumu washtakiwa hao wa kesi ya kula njama na kufanya maandamano isivyo halali kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kuwatia hatiani katika makosa yaliyokuwa yakiwakabili.
Washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo Februari 15 mwaka huu.
Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya tukio Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama za kufanya maandamano isivyo halali.
Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kusababisha uvunjifu wa amani.
Shtaka la tatu ilidaiwa kuwa washtakiwa wote kwa pamoja walikiuka amri ya Jeshi la Polisi ya kutoa zuio la kufanya maandamano, n a k u f a n y a mk u s a n y i k o uliosababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Katika shtaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.

No comments:

Post a Comment